Shindano La Uandishi Wa Hadithi
Tukiwa tunaelekea siku ya Kiswahili duniani, Mwanawetu Books and Consultancy imeandaa shindano la uandishi wa hadithi fupi kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari.
Mada: Kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani 2022 “SERIKALI YETU MADINI YETU”.
1.1. Maelezo kuhusu shindano
MBC inawakaribisha Wanafunzi wote wa Shule za Sekondari zilizopo katika mikoa ya Lindi, Mtwara, na Ruvuma; kushiriki katika shindano hili la Uandishi wa Hadithi fupi. Hadithi ziwe na maneno yasiyopungua mia mbili hamsini (250), na ziandikwe kwa mkono au kuchwapwa kwa mashine (kompyuta), michoro inaruhusiwa.
1.2. Jinsi Ya Kutumia Ikisiri
Ili kurahisisha mawasiliano; hadithi zote zitumwe zikiwa zina jina la Mwandishi (Mwanafunzi), jina la Shule anayosoma Mwandishi, kidato, namba za simu za Walimu wa Shule husika. Ni vema hadithi zikipitia kwenye ofisi ya uongozi wa Shule au idara ya lugha ya Kiswahili ya Shule husika.
Hadithi zitumwe kupitia barua pepe info@mwanawetubooks.co.tz au WhatsApp +255 737 966996 kuanzia tarehe 14 Februari, 2022 na mwisho wa kupokea hadithi ni tarehe 28 Februari, 2022.
1.3. Tunzo
Mshindi wa kwanza atapata zawadi ya fedha taslimu Tsh. 100,000/= pamoja na vifaa vya shule wakati washindi wengine 10 watapata zawadi mbalimbali pamoja na fedha taslimu.
Hadithi 10 bora zitachapishwa kwenye maktaba ya kidigitali inayopatikana mtandaoni kupitia tovuti; https://www.mwanawetubooks.co.tz
Washindi wote watatangazwa tarehe 08 Machi, 2022, katika sherehe ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
1.4 Siri ya ushindi
1. Kuhusianisha hadithi, wahusika, na kaulimbiu ya Siku ya Wanawake Duniani “Serikali yetu madini yetu”
2. Matumizi ya visawe visivyotumika mara kwa mara na Wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania
3. Mtiririko na mpangilio wa visa na wahusika
4. Uwezo wa kuhusianisha kaulimbiu na maisha halisi ya wanawake waishio katika ukanda wa madini
Kwa mawasiliano zaidi, wasiliana nasi kupitia;
Namba ya simu ya mkononi: +255 737 966996
Barua pepe: info@mwanawetubooks.co.tz