man

Posted by: Admin

2022-02-10
blog

Washindi Shindano La Uandishi Wa Hadithi

Lengo kuu la maktaba hii ya Mwanawetu Books ni kuenzi na kuiendeleza lugha ya Kiswahili, katika kutimiza lengo hili, MBC imeshirikisha Wanafunzi wa ngazi ya Shule za Sekondari kufanyia kazi mada walizosoma wakiwa shuleni kuhusu Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi.

Mada:
Inatokana na kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani 2022 “SERIKALI YETU MADINI YETU” ambayo imetumika na taasisi zilizopo katika Kanda ya Ziwa”.

Kwa nini kauli mbiu “Serikali Yetu, Madini Yetu” itumike Kanda ya Kusini?

Maeneo mengi ya Kanda ya Kusini yanaonekana kuwa na migodi mingi ya madini mbalimbali, migodi hiyo imeweza kunufaisha jamii nyingi za Kitanzania na nje ya nchi. Mfano wa migodi hiyo ni mgodi wa shaba ya bluu Tunduru mkoani Ruvuma, makaa ya mawe wilayani Mbinga, Nyasa.

Pia mkoani Lindi kuna migodi ya mawe ya gypsum wilayani Kilwa, gesi asilia Songosongo wilayani Kilwa na mgodi wa dhahabu na green tomalin wilayani Ruangwa, wakati mkoa wa Mtwara ukiongozwa na uchimbaji mkubwa wa gesi asilia na uzalishaji wa chumvi na chokaa.

1.1. Tunzo
Mshindi wa kwanza atapata zawadi ya fedha taslimu Tsh. 100,000/= pamoja na vifaa vya shule wakati washindi wengine 10 watapata zawadi mbalimbali pamoja na fedha taslimu.

Hadithi 10 bora zitachapishwa kwenye maktaba ya kidigitali inayopatikana mtandaoni kupitia tovuti; https://www.mwanawetubooks.co.tz
Washindi wote watatangazwa tarehe 08 Machi, 2022, katika sherehe ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

1.2. Siri Ya Ushindi

1. Kuhusianisha hadithi, wahusika, na kauli mbiu ya Siku Ya Wanawake Duniani “Serikali Yetu Madini Yetu”
2. Matumizi ya visawe visivyotumika mara kwa mara na Wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania.
3. Mtiririko na mpangilio wa visa na wahusika.
4. Uwezo wa kuhusianisha kaulimbiu na maisha halisi ya wanawake waishio katika ukanda wa madini.

Kwa mawasiliano zaidi, wasiliana nasi kupitia;

Namba ya simu ya mkononi: +255 737 966996
Barua pepe: info@mwanawetubooks.co.tz