02 May
2022Lengo kuu la maktaba hii ya Mwanawetu Books ni kuenzi na kuiendeleza lugha ya Kiswahili, katika kutimiza lengo hili, MBC imeshirikisha Wanafunzi wa ngazi ya Shule za Sekondari kufanyia kazi mada walizosoma wakiwa shuleni kuhusu Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi.
Mada: Inatokana na kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani 2022 “SERIKALI YETU MADINI YETU” ambayo imetumika na taasisi zilizopo katika Kanda ya Ziwa.
Maeneo mengi ya Kanda ya Kusini yanaonekana kuwa na migodi mingi ya madini mbalimbali, migodi hiyo imeweza kunufaisha jamii nyingi za Kitanzania na nje ya nchi. Mfano wa migodi hiyo ni mgodi wa shaba ya bluu Tunduru mkoani Ruvuma, makaa ya mawe wilayani Mbinga, Nyasa. Pia mkoani Lindi kuna migodi ya mawe ya gypsum wilayani Kilwa, gesi asilia Songosongo wilayani Kilwa na mgodi wa dhahabu na green tomalin wilayani Ruangwa, wakati mkoa wa Mtwara ukiongozwa na uchimbaji mkubwa wa gesi asilia na uzalishaji wa chumvi na chokaa.
Mshindi wa kwanza amepata zawadi ya fedha taslimu Tsh. 100,000/= pamoja na vifaa vya shule wakati washindi wengine 10 wamepata zawadi mbalimbali pamoja na fedha taslimu.
Hadithi 10 bora zitachapishwa kwenye maktaba yetu ya kidigitali inayopatikana mtandaoni kupitia; https://www.mwanawetubooks.co.tz
Washindi wote walitangazwa tarehe 08 Machi, 2022, katika sherehe ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
1. Uwezo wa kuhusianisha hadithi, wahusika, na kaulimbiu ya Siku ya Wanawake Duniani “Serikali
yetu madini yetu”
2. Matumizi ya visawe visivyotumika mara kwa mara na Wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili
nchini Tanzania
3. Mtiririko na mpangilio wa visa na wahusika
4. Uwezo wa kuhusianisha kaulimbiu na maisha halisi ya wanawake waishio katika ukanda wa
madini
NOVEMBER 06, 2021
Very interesting story, thanks to the author of "Usimuache Atoke"
ReplyNOVEMBER 06, 2021
We need more of these stories for learning in a day to day life
ReplyNOVEMBER 06, 2021
More book stories to come and we are working on bringing more to our audience for further learning and self development
ReplyCopyrights © 2022-mwanawetubooks.co.tz - All Rights Reserved
Write Your Review